Taharuki za ubaguzi zakithiri Afrika kusini



Kijana wa miaka 15 na mwenzake wa miaka 21 wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo katika eneo la Ventersdrop wakishtumiwa kuhusika na mauaji ya mzungu aliyetetea sera za ubaguzi wa rangi Eugene Terre'Blanche.
Kumeuwepo na uhasama baina ya raia wa kizungu na weusi kufuatia mauji hayo, na wachambuzi wanasema huenda kufunguliwa kwa kesi hiyo kukatuliza uhasama huo.
Mwanasiasa huyo alikatwakatwa hadi kufa hapo Jumamosi usiku katika makaazi yake.
Polisi wanasema mauji ya Terre'Blanche katika shamba lake yalifuatia mzozo kuhusu malipo ya wafanyakazi.
Lakini wafuasi wake wanalaumu uchochezi wa kiongozi wa vijana wa ANC, Julius Malema kuwa chanzo cha mauji yake. http://www.bbcswahili.com/

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment