MHARIRI mwanzilishi wa gazeti la MwanaHALISI na mwanahabari mwandamizi, ARISTARIKO KONGA (49) amefariki dunia juzi jijini Dar es Salaam.Konga alifariki dunia katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa kwa muda wa wiki mbili.
Zaidi ya kuwa mhariri mwanzilishi wa MwanaHALISI, Konga alifanya kazi pia katika nafasi mbalimbali katika vyombo tofauti vya habari nchini— vya serikali na vile vya binafsi.Mbali ya MwanaHALISI linalomilikiwa na kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited (HHPL), Konga aliwahi kufanya kazi MAELEZO, Business Times Limited, Habari Corporation Limited, Mwananchi Communications Limited, The Guardian Limited na Raia Mwema.
Kwa ufupi, Konga ni miongoni mwa waandishi wachache nchini waliowahi kupata fursa ya kufanya kazi katika magazeti yote makubwa hapa nchini na kutoa mchango mkubwa.
Msiba uko nyumbani kwa marehemu Ubungo Kibo jirani na baa ya Mpembene jijini Dar es Salaam. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda mkoani Iringa kwa mazishi.Konga alizaliwa mwaka 1961 katika kijiji cha Makusi, Kata ya Mlondwe, Tarafa ya Matamba, Wilaya ya Makete, mkoani Iringa. Ameacha mjane na watoto watatu.
Saed KubeneaMkurugenzi Mtendaji
0 comments:
Post a Comment