TAARIFA MUHIMU KWA VYOMBO VYA HABARI!!

Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Abdallah Mssika.

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi


Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Kuratibu Silaha ndogondogo hapa nchini, Jumanne Aprili 27, 2010 saa 2.00 asubuhi itakutana ili kupitia maazimio ya mapendekezo ya mshwaada wa kurekebishaji sheria za kumiliki silaha hapa nchini.

Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Abdallah Mssika, amesema kuwa Mkutano huo ambao utafanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kuanzia saa 2.00 asubuhi, utawashirikisha baadhi ya Maafisa wa Wizara na Idara za Serikili zinazojihusisha na masuala ya kiusalama pamoja na baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mkutano huo ambao pia utahudhuriwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai utafunguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Lawrence Masha.

Kutokana na umuhimu na uzito wa masuala yatakayozungumziwa siku hiyo, Wahariri mnaombwa kutuma waandishi na wapiga Picha kwa ajili tukio hilo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment