Somalia yakamata wahamiaji haramu raia wa Ethiopia!!


Maafisa wa eneo lilnalojiita Puntland, kaskazini mashariki mwa Somalia wamesema wamewatia mbaroni zaidi ya wahamiaji haramu mia moja kutoka Ethiopia.
Wahamiaji hao wamekamatwa kufuatia msako wa siku mbili katika maeneo ya pwani ya eneo hilo.
Waziri wa Usalama wa Puntland, Yusuf Ahmed Kheyr, alisema hatua hiyo ni ujumbe uliowazi kwa wale wanaojinufaisha na maisha wanadamu.

Kauli ya waziri huyo inahusiana na madai ya kuwepo kwa makundi ya watu kutoka Puntland, kujihusisha na usafirishaji wa wahamiaji haramu kutoka Ethiopia na eneo la kusini mwa Somalia.
Wahamiaji hao wakishafika Puntland huvuka Ghuba ya Aden kuelekea Yemen, wakiwa na matumaini ya kufika Saudi Arabia.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment