Safari za ndege kukwama Ulaya yashutumiwa!!


Mashiirika ya kimataifa ya ndege yamewashtumu vikali maafisa wakuu wa muungano wa ulaya kwa namna walivyokabiliana na tisho la kusambaa kwa wingu la majivu ya volcano nchini Iceland.

Mashirika hayo yanasema hatua ya kusimamisha safari za ndege katika baadhi ya nchini Ulaya ni ya kupotosha na imesababisha athari kubwa kwa sekta hiyo.

Viongozi wa Ulaya pia wameshtumiwa kwa kutochukua hatua ili kutatua matatizo ya usafiri. Mashirika hayo ya ndege yametaja usumbufu uliosababishwa na kufutwa kwa safari za ndege kama aibu kubwa.

Hatahivyo siku tano baada ya matatizo hayo kuanza Kamishna wa safari za ndege barani Ulaya Siim Kallas amesema swala la usalama halina mjadala. Amesema mashirika ya ndege ndiyo yanapaswa kushugulikia maslahi ya abiria waliokwama.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment