Mwanamuziki wa HipHop anayeheshimika kwa mashairi yake yenye ujumbe mkali katika masuala mbalimbali katika jamii Joseph Haule Prof. J. inasemekana yuko Studio kwa sasa akirekodi nyimbo kadhaa kwa ajili ya kuibuka na albam yake mpya ambayo bado haijajulikana itapewa jina gani.
Akizungumza na Kamanda kiongozi wa FULLSHANGWE meneja wa mwanamuziki huyo anayejulikana kwa jina la Eliana amesema tayari ameshaanza kurekodi nyimbo kadhaa katika studio za Tongwe Records kwa producer Lamaa, lakini pia atafanya kazi na maproducer wengine kama vile Hamy B., P. Funk na wengine wengi ili kuiboresha zaidi albam hiyo inayotarajiwa kukamilika hivi karibuni.
Eleana amesema katika albam hiyo Prof J. anatarajia kuwashirikisha nyota kadhaa wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini na Afrika Mashariki kama vile Belle Nine, Mwana FA, na Ambwene Yesaya AY ambapo pia sauti kadhaa za wanamuziki wakali katika nchi za Kenya na Uganda zinatarajiwa kusikika katika albam hiyo.
Eleana hakuzitaja nyimbo lakini akasema mambo yanaendelea vizuri na wakati wowote kuazia wiki ijayo ataweka hadharani baadhi ya mambo ambayo yatakuwa yamekamilika ikiwemo majina ya nyimbo mbili ambazo zinarekodiwa kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment