Kiongozi wa kanisa la Kianglikana duniani, Dr Rowan Williams, amesema Kanisa Katoliki nchini Ireland limepoteza "uaminifu wake wote" kutokana na jinsi lilivyoshughulikia suala la makasisi wanaodaiwa kuwadhulumu watoto kimapenzi.
Dr Williams alisema matatizo ya kanisa hilo yaliathiri jamii kwa vile yalisababisha kiwewe kikubwa.
Akizungumza na BBC, alisema madai ya dhulma za kimapenzi dhidi ya watoto yaliwafanya maaskofu washindwe kuonekana hadharani.
Hii ni mara ya kwanza kwa Dr Williams kuzungumzia kashfa hii.
Kashfa hii imezusha utata kuhusu namna Papa Benedict alivyoshughulikia shutuma za watoto kudhulumiwa kimapenzi na makasisi, kabla ya kuwa Papa wa kanisa Katoliki.
Lakini wafuasi wake wamesema Papa alitoa kanuni kadhaa za kuwalinda watoto.

0 comments:
Post a Comment