Habari zilizotufikia punde ambazo bado hazijathibitishwa na Wahusika zinasema Mnenguaji mahiri na wa Siku nyingi aliyewahi kufanya kazi katika bendi tofauti hapa nchini na Falme za Kiarabu Diana Astone Villa amefariki dunia leo asubuhi.
Inasemekana msiba uko nyumbani kwake Buguruni alikokuwa akiishi inasemekana aliugua kwa muda mrefu na hivi karibuni Diana alilazwa katika hospitali ya Amana Ilala jijini Dar es salaam, FULLSHANGWE inaendelea kufuatilia habari hizi na mara itakapopata habari zaidi itawajulisha mara moja wadau
0 comments:
Post a Comment