Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
Mtoto wa Malkia wa Uholanzi, Her Royal Highness Princenss Maxima, kesho mchana atatembelea Kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi hapa nchini kukagua maendeleo ya mradi wa ukarabati wa majengo ya Hospitali hiyo.
Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Msaidizi ACP Abdallah Mssika, amesema kuwa Bi. Maxima ambaye atafuatana na ujumbe wa watu 30 kutoka idara na wizara mbalimbali za nchini Uholanzi atakuwa hapa nchini kwa ziara ya siky tatu.
Amesema akiwa kwenye Hospitali ya Jeshi la Polisi Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam, Bi Maxima, pia atakutana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Lawrence Masha na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jeneralki Saidi Mwema, pamoja na Maafisa Wakuu wa Jeshi la Polisi akiwemo Kamanda wa Kikosi cha Polisi Afya DCP Nelvin Mashayo.
Serikali ya Uholanzi kupitia Shirika lake la Maendeleo linalohudumia miradi ya Afya kwa nchi za Afrika, Farm Access International (PAI) imegharimia ukarabati wa Vituo vya Afya vya Jeshi la Polisi katika mikoa ya Mwanza, Mbeya, CCP Moshi Mkoani Kilimanjaro, Zanzibar, Arusha, Tabora, Dodoma na Makao Makuu ya Kikosi hicho Jijini Dar es Salaam.
Kamanda Mssika amesema kuwa tayari ukarabati katika Hospitali za Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, CCP na Zanzibar umeshakamilika na Hospitali nyingine za Polisi katika mikoa ya Arusha, Tabora na Dodoma uko katika hatua mbalimbali.
Amesema kwa mujibu wa Kamanda wa Kikosi cha Polisi Afya hapa nchini Naibu Kamishna DCP Neven Mashayo, tayari ukarabati huo umeshaghalimu zaidi ya shilingi milioni 700.
Amesema Shirika hilo limeshafanya ukarabati wa majengo ya Kitengo cha huduma za tiba ya Ukimwi VCT na maabara ya kisasa ya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali yakiwemo ya Kifua Kikuu (TB) na Kiliniki kwa akina mama walioathirika na virusi vya HIV pamoja na sehemu maalumu ya uteketezaji wa taka zitokanazo na Hospitali hiyo.
0 comments:
Post a Comment