Kampuni ya Mashujaa Entertainment Group ya jijini Dar es Salaam imeshangazwa na Vipaji walivyonavyo wasanii wa Muziki wa bendi ya Mashujaa Musica inayoendelea kufanya maonyesho yake sehemu mbalimbali za jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Mamaa Sakina(Cash Lady), amewapongeza kutokana na mwenendo mzuri wa sanaa yao ambayo anasema wakiendelea hivyo wataweza kufika mbali ikiwa ni pamoja na kujipatia kipato na kuweza kujitangaza wao wenyewe kimuziki.
“ni kinyume na matarajio yetu kwani hatukutarajia kama wasanii hawa wanauwezo mkubwa kiasi hiki ambapo kama unavyosikia tangu waunde kundi hili la Mashujaa pamoja na kwamba ni muda mfupi lakini kazi zao zimeendelea kuonekana ikiwa ni pamoja na kusikiwa katika vituo mbalimbali vya Radio, na kazi zao zimeonekana ni wabunifu wazuri wa masuala ya muziki”alisema Mamaa Sakina.
Aidha Sakina amewataadhalisha wale wote wanaotaka kwenda kinyume na taratibu za kazi kwamba huu sio wakati wa kuanzisha taflani isipokuwa wakazane katika kutengeneza mazingira mazuri ikiwa ni pamoja na kujenga mahusiano mema wao na wenzao ili kuondokana na tatizo la kuonekana wengine kuwa bora zaidi ya wengine.
“Tabia ya Mtu ndiyo kielelezo chema wakati wote machoni pa watu, ukiwa na tabia njema siku zote utapendwa na watu wote, kwani kumbuka kwamba Chema chajiuza na kibaya chajitembeza, siku zote nawhusia wanangu hawa kuwa na tabia njema popote ili waweze kuziuza kazi zao kwa mashabiki wanaowazunguka, pia itawaongezea nafasi ya maisha bora kwani penye nia pana njia, hivyo kila mmoja napenda kumwambia kwamba wakazane na kujiwekea malengo ili waweze kufia”alisema Sakina
Hata hivyo aliwaonya kutojiingiza katika biashara mbaya ikiwemo vitendo vya Uvutaji wa Madawa ya Kulevya, Bangi, Umalaya na Ukahaba kwamba ni vitendo vinavyoharibu maisha ya wasanii wengi kutokana na kulewa sifa.
Mashujaa Musica ni Bendi Mpya ambayo imeundwa mwaka huu na tangia kuundwa imeweza kufikia mafanikio makubwa kwa muda mfupi hata kufikia kuliteka jiji la Dar es Salaam na Vitongoji vyake baada ya kutelemsha vibao viwili ambavyo mashabiki kote nchini waliobahatika kusikia na kutazama katika televisheni wameweza kushuhudia jinsi bendi hiyo inavyokuja kwa kasi hata kuwaweka roho juu baadhi ya wamiliki wa bendi kubwa zikiwemo za Twanga, Fm Academia na Acudo Impact.
Mashujaa Musica kwa sasa ipo chini ya uongozi wa Elystone Angai anayesaidiwa na Jado Fidifosi makao makuu yake yakiwa ni Eneo la Vingunguti Kiembe Mbuzi, ambapo Ukumbi wake wa Nyumbani ukiwa ni Mashujaa Pub uliopo katikati ya Vingunguti.
0 comments:
Post a Comment