JAMBAZI LAUAWA KATIKA MAPAMBANO NA POLISI!!

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi

TARIME JUMATANO APRILI 07, 2010. Jeshi la Polisi katika Mkoa maalumu wa Kipolisi wa Tarime- Rorya limepamba na Majambazi yenye silaha aina ya SMG na kufanikiwa kuliua moja kwa risasi na kuokoa ng’ombe 11 zilizokuwa zimeibwa nchini Kenye.
Kamanda wa Polisi mkoani humo SSP Costantine Masawe, alisema kuwa tukio hilo limetokea jana usiku huko kwenye eneo la Vijiji vya Ganyange na Kimusi wilaya ya Tarime baada ya kupata taarifa kutoka kwa wenzao wa Polisi Kenya kuwa kuna majambazi yaliyopora mifugo na kuelekea upande wa Tanzania.

Kamanda Massawe alisema mara baada ya kupata taarifa hizo Polisi walijipanga na kuelekea katika maeneo yanayosadikiwa kuwa ni mapito ya wezi wa mifugo hiyo na ndipo wakiwa katika maeneo ya kijiji cha Nyantira kata ya Muriba majambazi hayo yalijitokezai na kuingia katika mtego Polisi na walipotakiwa kujisalimisha walikaidi amri hiyo na kuanza kuwashambulia Polisi kwa risasi.
Hata hivyo Kamanda Masawe amesemna kuwa baada ya majibizano makali ya risasi kwa muda kadhaa, Polisi waliweza kuyashambulia majambazi hayo na kumuua mmoja na kupata silaha hatari aina ya SMG yenye namba 56131517 ikiwa na risa.
Kamanda Massawe alisema kuwa mwili wa jambazi huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Serikali ya wilaya Tarime na ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kwenda kulitambua jambazi hilo.
Hata hivyo Kamanda Masawe amesema kuwa bado Polisi wanaendelea na operesheni ya kupambana na wahalifu mbalimblia wakiwemo wa kilimo cha zao haramu cha bangi na upikaji na uuzaji wa pombne haramu ya gongo.
Operesheni hiyo inafanyika chini ya Mkuu wa Operesheni Maalum za Jesdhi la Polisi nchini Naibu Kamishna DCP Venance Tossi, akisaidiwa na Maafisa wengine waandamizi kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Jijini Dar es Salaam DCP Simon Kasala na Mkuu wa Interpol hapa nchini SACP Hussein Nassoro Laiser.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment