Mchezaji wa Manchester United Nani akishangilia mara baada ya kupachika goli wakati wa mchezo katika ya Man U. na Totenham.
Timu ya Manchester United ya Uingereza leo imeichapa bila huruma timu ya Totenham magoli matatu kwa moja na kufikisha pointi 79 katika msimamo wa ligi hiyo katika mchezo wa ligi kuu ya nchi hiyo Premier Liegue uliomalizika hivi pinde.
Magoli ya Manchester Unitedi yamefungwa na wachezaji Rayn Gigs katika dakika ya 78 na 85 kipindi cha pili magoli mawili yote kwa njia ya penati wakati pia Nani amefunga goli moja na kukamilisha idadi ya magoli matatu hivyo kujikita zaidi kileleni mwa ligi hiyo.
Totenham wamejipatia goli moja kupitia mchezaji wao Ledley King katika dakika ya 71 ya mchezo huo, hata hivyo kupatikana kwa goli hilo bado hakukuisaidia Totenham kupata ushindi hivyo ikazama mbele ya wenyeji Manchester United kjwenye uwanja wa Oldtraford.
0 comments:
Post a Comment