Afisa wa shirika la kutetea haki anyimwa kibali Rwanda!!



Mwakilishi wa shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch nchini Rwanda amenyimwa kibali cha kufanya kazi na anapaswa kuondoka nchini humo.

Waziri wa mambo ye nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo, aliIambia BBC kuwa nyaraka za afisa huyo za maombi ya kibali cha kazi hazikujazwa vizuri.

Bi Mushikiwab amesema kuwa shirika hilo lina historia ya kutoa repoti zinazopendelea upande mmoja.

Uchaguzi unatarajiwa kufanyika nchini Rwanda katika kipindi cha miezi minne, na magazeti yote huru yamefungwa huku vyama vya kisiasa vikikataliwa usajili.

Mwanasiasa mmoja wa upinzani, Victoire Ingabirre Umuhoza, anayetarajia kugombea urais amewekwa chini ya ulinzi mkali baada ya kushutumiwa kushirikiana na magaidi. www.bbcswahili.com

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment