Makamu Mwenyekiti wa Bunge la china atembelea bunge la Tanzania!!

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Jan Junqi katika chakula cha jioni alichoandaliwa na Spika wa Bunge , Samuel Sitta kwenye hoteli ya Mtakatifu Gasper Mjini Dodoma, Aprili 19, 2010, Wapili kulia ni Spika wa Bunge Samuel Sitta . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mizengo Pinda akifurahia jambo katika mazungumzo kati yake na Mbunge wa Busanda, Lolesia Bukwimba (kulia) na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa (kushoto) kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 20, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Makamu Mwenyekiti wa Bunge la china Mhe. Yan Junqi akisisitiza jambo katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika Ofisi ya Spika Bungeni kati ya Ujumbe wa Tanzania kwa kuongozwa na Mhe. Spika. Kulia ni Balozi wa China nchini Mhe. Liu Xinsheng na kushoto ni Mkalimani wa ujumbe huo Bi. Shi Meiqi. Makamu Mwenyekiti huyo wa Bunge la china , yupo nchini kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine, ziara yake inakusudia kuimarisha ushirikiano kati ya Bunge la China na Tanzania. Picha na Owen Mwandumbya.

Spika wa Bunge Samuel Sitta akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Spika wa Bunge la China, Mhe.. Jan Junqi katika chakula cha jioni alichomwandalia mgeni huyo kwenye hoteli ya Mtakatifu Gaspar Mjini Dodoma Aprili 19, 2010. (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Spika wa Bunge Samuel Sitta akimkabidhi zawadi, Naibu Spika wa Bunge la China, Mhe. . Jan Junqi katika chakula cha jioni alichomwandalia mgeni huyo kwenye hoteli ya Mtakatifu Gaspar Mjini Dodoma Aprili 19, 2010. (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wasanii wakicheza ngoma ya Hiyari ya Moyo katika chakula cha jioni alichoandaliwa Naibu Spika wa Bunge la China, Mhe. Jan Junqi kwenye hoteli ya Mtakatifu Gaspar Mjini Dodoma Aprili 19, 2010.
Naibu Spika wa Bunge Anna Makinda (kush) akijadili jambo leo bungeni na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Maheabu wa Serikali Ludovic.(Picha na Mwankombo Jumaa -MAELEZO)

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment