HASSAN DALALI AENGULIWA UCHAGUZI SIMBA, HATA HIVYO ATAKUMBUKWA KWA MAFANIKIO YAKE!!

Mwenyekiti wa Simba Hassan Dalali akilia huku akifarijiwa na shabiki wa Simba baada ya ushindi mnono jana dhidi ya timu ya Yanga hata hivyo kamati ya uchaguzi imemwengua leo katika kinyang'anyiro cha kugombea Uwenyekiti Simba.

Kamati ya uchaguzi ya Simba leo imewatema wagombea uenyekiti wawili wa timu hiyo katika mchujo wa uchaguzi uliofanyika katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF unaotarajiwa kufanyika mei 9 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Waliotemwa katika mchujo huo ni Mwenyekiti wa zamani Hassan Dalali na mgombea mwingine Mohamed Nyali hivyo waliobaki katika kinyang'anyiro hicho ni Michael Wambura, Aden Rage, Hassan Hasanoo na Hanspope.

Katika Nafasi ya Makamu mwenyekiti wagombea wawili aliyekuwa katibu mkuu wa Simba Mwina Kaduguda na Geofrey Nyange (Kaburu) wamepitishwa kugombea nafasi hiyo bila matatizo.

Katika nafasi ya ujumbe wagombea kumi na saba waliomba na wagombea saba wametoswa huku wakibaki wagombea kumi kuendelea na kinyang'anyiro hicho usaili huo umefanyika karibu siku nzima ya leo na kamati ya uchaguzi ambapo ulipitia nyaraka mbalimbali za wagombea walizowasilisha ili kuonyesha sifa za kugombea nafasi hizo lakini pia kamati hiyo imepitia pingamizi mbalimbali zilizowasilishwa na na baadhi ya wanachama wa Simba dhidi ya baadhi ya wagombea.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. acheni ubwege simba kawaongoza siku zote hamkujua kama hajasoma naubingwa kawaletea sasa chagueni majambazi muone kazi

Post a Comment