Wanajeshi Madagascar wadaiwa kupanga mapinduzi!


Wanajeshi saba na raia wawili wamekamatwa nchini Madagascar kwa shutma za kupanga njama ya mapinduzi.

Afisa mmoja wa usalama amesema washukiwa hao walikuwa wakipanga kushambulia ofisi wa waziri mkuu katika mji mkuu, Antananarivo.Amesema nia yao ilikuwa kuua ili kusababisha mgawanyiko katika jeshi la Madagascar.

Mapema mwezi huu waziri mkuu Camille Vital alimfuta kazi waziri anayehusika na maswala ya kijeshi baada ya kufanya mkutano na wakuu wa jeshi bila kumfahamisha.

Jeshi la Madagascar lilimsaidia kiongozi wa sasa, Andry Rajoelina, kujipatia mamlaka baada ya mapinduzi ya mwaka jana.

www.bbcswahili.com

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment