Hanbari zaidi juu ya kifo cha Diana Aston Vila zinasema alifariki leo asubuhi saa moja katika Hospitali ya Amana alikokuwa amelazwa na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali hiyo mpaka utakapochukuliwa kwa mazishi yatakayofanyika nyumbani kwa baba yake Kigogo Mbuyuni jijini Dar es salaam.
Mpaka sasa msiba uko nyumbani kwake alikokuwa akiishi Buguruni Malapa na inasemekana mama yake mzazi hajaongea na mwandishi yeyote pengine inawezekana ni kutokana na mshtuko wa kuondokewa na mwanaye kipenzi
Diana Aston Villa atakumbukwa katika sanaa ya muziki hasa katika unenguaji kwani alikuwa mahiri na alifanya kazi katika bendi nyingi nchini kama vile Diamond Musica enzi hizo, African Stars na pia aliwahi kufanya kazi na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya uliojulikana kama TAKEU, Mr Nice aliyewika sana miaka ya hivi karibuni, Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Diana Aston Villa -AMIN
0 comments:
Post a Comment