Chama kimoja muhimu cha upinzani nchini Sudan kimemtaka Rais Omar al-Bashir kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki unafanyika nchini humo mwezi huu.
Hata hivyo, chama hicho cha Umma kutoka eneo la kaskazini, kinachoongozwa na waziri mkuu wa zamani Sadiq al-Mahdi kimeweka masharti kadhaa ambayo kinataka yatekelezwe ifikapo siku ya Jumanne, kabla ya kukubali kushiriki uchaguzi.
Baada ya mazungumzo na mjumbe maalum wa Marekani nchini Sudan, Scott Gration, chama cha Umma kilisema kinataka uchaguzi uahirishwe kwa majuma manne, kupatiwa nafasi ya kutumia vyombo vya habari vya serikali, na kuundwa kwa chombo kipya kitakachosimamia uchaguzi.
Vyama vingi vinavyompinga Rais Omar al-Bashir viliwaondoa wagombea wake wa kiti cha urais kutokana na wasiwasi wa hali ya usalama pamoja na uwezekano wa kutokea kwa wizi wa kura.
Rais Bashir, ambaye anatakikana na mahakama ya kimataifa kwa madai ya uhalifu wa kivita katika jimbo la Darfur, amekuwa akipinga wazo la kuahirisha uchaguzi huo, ambao ni wa kwanza wenye kushirikisha vyama vingi kufanyika nchini humo kwa kipindi cha miaka 24 sasa.
0 comments:
Post a Comment