1: Kwamba Notisi iliyotolewa ni ya Mgomo usiohalali kwa kuwa sababu za mgomo hazipo.
(a)Njia za Majadiliano bado zipo wazi na wala majadiliano hayajafungwa wala kushindikana.
(b)Mgomo uliotangazwa hauna kipindi maalum kinyume na matakwa ya kisheria.
(c)Mgomo uliotangazwa unahusu sekta zote za uchumi wa nchi ikiwemo sekta binafsiambayo ina taratibu zake za kuhakikisha na kulinda maslahi ya wafanyakazi.
(d)Mgomo huu utahusu pia sekta ya huduma muhimu kwa jamii (essential Servises) ambazo haziruhusiwi kisheria kugoma.
2:Kwakuwa mgomo huu si halali waajiri watakaoathirika watakuwa na haki ya kuwachukulia hatua za kinidhamu wafanyakazi watakaoshiriki mgomo haramu ikiwemo kuwafukuza kazi, kutokuwalipa mishaharakwa kipindi cha mgomo na hata kuajiri wafanyakazi mmbadala,. Ijulikane kwa kwa wadau wote kwamba sheria zilizopo hazilindi wafanyakazi wanaoshiriki mogomo haramu.
3: Iwapo mgomo huu utatekelezwa waajiri watakaoathirika watakuwa na haki ya kudai fidia kwa hasara itakayosababishwa na mgomo huodhidi ya TUCTAiliyoitisha mgomo usio halali.
4: Tunatoa RAI kwa TUCTA na wadau wote waliohamasishwa na TUCTA, waachane na harakati za kuitisha mgomo usio halali na ambao utakuwa ni hasarakwa pande zote. TunaisihiTUCTA washiriki kwa dhati majadiliano yenye lengo la kuleta muafaka wa pamoja, kwa hili hakuna njia ya mkato. TUCTA itambue kwamba majadiliano baina ya wadau yanajengahali ya kuaminiana na mahusiano mazuri endelevu.
Ikumbukwe kwamba amani na utulivusehemu ya kazi ni nguzo muhimu za kuongeza na kukuza uchumi na tija kazini, kuwepo kwa ajira endelevu na kupambana na umasikini , Vyam,a vya wafanyakazi ni wadau muhimu katika kuendeleza amani na utulivu mahali pa kazi, walioko katika picha katikati ni Wakili Cornellius Kariwa Mwenyekiti wa chama cha waajiri ATE na mwisho kulia ni Afisa habari mwandamizi Maelezo Cisse Mwirabi.
0 comments:
Post a Comment