Mwanachama wa Simba na aliyewahi kuwa mwenyekiti wa muda wa Klabu hiyo Richald Wambura ametangaza kuchukua fomu hii leo wakati alipozungumza na waandishi wa habari kwenye Klabu ya Break Point Posta jijini Dar es salaam wambura amesema nia ya kugombea anayo na uwezo wa kuiongoza klabu hiyo pia anao.
Klabu ya Simba ilitangaza kutoa fomu kwa wagombea wa nafasi za Mwenyekiti na Makamu wake na tayari fomu hizo zimeanza kutolewa katika makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi Kariakoo na mwisho wa kutoa fomu na kurejesha itakuwa tarehe 10 mwezi aprili wakati uchaguzi wa klabu hiyo unatarajiwa kufanyika Mei 9.
Mpaka sasa wanasimba waliochukua fomu ni Meina Kaduguda Makamu mwenyekiti,Jofrey Nyange Kaburu, na Mwenyekiti ni Aden Rage na Wambura ambaye leo ndiyo ametanabaisha kugombea nafasi hiyo.
0 comments:
Post a Comment