Meneja Masoko wa Zantel, Rweyemamu Protace (kulia) akifafanua jambo kuhusu promosheni hiyo,akiwa na Meneja Masoko wa Mkoa wa Tanga Nassor Mbilikira katika uzinduzi huo.
Kampuni ya Simu za mkononi nchini, Zantel, siku ya Ijumaa ya tarehe 19, Machi 2010, ilizindua promosheni ya CHOMOKA NA VYOMBO maalum kwa wakazi wa Tanga. Promosheni hiyo itawawezesha wateja wa zantel mkoani Tanga kupata nafasi ya kujishindia vyombo vya ndani kila wiki kwa muda wa wiki 8. Mgeni rasmi katika hafla hiyo fupi ya uzinduzi alikuwa Meya wa Jiji la Tanga Mstahiki Kassim Kisauji ambaye aliishukuru Zantel kwa kusambaza mtandao wake hadi Tanga na kuwapa fursa wakazi wa jiji lake kujishindia zawadi nzuri.
0 comments:
Post a Comment