Google kutodhibiti wavuti zake China!!


Uchina imeghadhabishwa na tangazo la kampuni ya GOOGLE, kukoma kudhibiti mitandao ya internet ya tafuta tafuta inayotumika kwa lugha ya kichina.
Uamuzi wa kampuni ya GOOGLE kufunga mtandao wake rasmi wa tafuta tafuta nchini Uchina , ni pigo kubwa kwa sifa ya nchi hiyo kimataifa.
Google ambayo ni kampuni mashuhuri, imesema haiko tayari kushirikiana na Uchina katika kudhibiti internet.
Ni wazi kuwa serikali hiyo ya kikomunisti ilitaka Google ibane taarifa muhimu ikiwa ilitaka kuendesha huduma zake nchini humo.
Na sasa Google inasema haiko tayari kutii masharti hayo hususan baada ya serikali kuanza kudhibiti uhuru wa kujieleza kupitia mitandao, huku baadhi ya blogu na akaunti za wanaharakati zikivamiwa nchini humo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment