Polisi Kenya wahusishwa na kutoweka kwa gaidi!

Kenya imewasimamisha kazi maafisa wake watatu wa polisi kufutia kutoroka rumande kwa mshukiwa mmoja anayedaiwa kuwa na uhusiano na kundi la wanamgambo wa kisomali la Al Shaabab.
Jamaa huyo Hussein Hashi Farah, mwenye asili ya Somalia na uraia wa Australia alikamatwa mapema mwezi huu, lakini akatoroka saa kadhaa kutoka gereza moja mjini Busia magharibi mwa Kenya.
Inaaminika Bwana Farah alitorokea Uganda ambako aliingilia saa kadhaa kabla ya kukamatwa.
Polisi wanawashikilia wafanyabiashara wawili wa kenya waliomtembelea bwana Farah muda mfupi baada ya kuwekwa rumande.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment