WATATU WAFA KATIKA AJALI , 12 WAJERUHIWA, WA 4 HOI BIN TAABAN!!


Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
Watu watatu wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa vibaya katika ajali tatu tofauti za Barabarani zilizotokea jana katika mikoa ya Tabora, Shinyanga na Pwani.
Mkoani Tabora, mtu mmoja amefariki na wengine 12 kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea kwenye barabara Kuu ya Igunga- Nzega mkoani humo.
Akizungumzia ajali hiyo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Tabora SSP Anthony Ruta, amesema kuwa ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 11.00 jioni kwenye kijiji cha Nanga eneo la Mlima Pasua katika Barabara ya Kuu ya Igunga-Nzega.
Amesema ajali hiyo imetokea baada ya Lori moja lenye namba za usajili T435 BCC likiwa na tela namba T 483 BBE likiendeshwa na Ali Ellye(35) kuigonga gari nyingine yenye namba T 489 AKY aina ya Isuzu Canter iliyokuwa ikiendeshwa na Salum Ali(32).
Kamanda Ruta amemtaja mtu mmoja aliefariki katika ajali hiyo kuwa ni utingo wa gari la Isuzu Rashidi Saidi(29), mkazi wa kijiji cha Mwisi Igunga mkoani Tabora.
Amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Kurwa Mohammedi(32) mfanyabiashara na kukazi wa Kijiji cha Simbo, Samweli Kuyeye(60) mkazi wa Nkinga, Lucas Mhindwa(29) wa Uswaya, Maduhu Shija(42) mkazi wa Mwisi, Charles Mahita(30) mkazi wa Simbo, Shija Kudelia(60) mkazi wa Mwisi.
Wengine waliojeruhiwa ni Salum Ali(32) mkazi wa Simbo ambaye ni dereva wa Canter na Joseph Makalanga(27) mkazi wa Uyuwi mjini Tabora, Michael Machibya(63) mkazi wa Kijiji cha Nkinga, Hassan Manua (23) mkazi wa Mwisi, Gilaya Butondo(30) mkazi wa Mwisi, Mabula Jackson(22) mkazi wa Meatu mkoani Shinyanga,
Kamanda Ruta amesema majeruhi wanne kati ya hao hali zao ni mbaya na wamelazwa katika Hospitali ya Misheni ya Nkinga wilayani Igunga kwa matibabu.
Amewataja majeruhi hao kuwa ni Michael Machibya(63) mkazi wa Kijiji cha Nkinga, Hassan Manua (23) mkazi wa Mwisi, Gilaya Butondo(30) mkazi wa Mwisi, Mabula Jackson(22) mkazi wa Meatu mkoani Shinyanga.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment