Na Moahammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
Wakuu wa Majeshi ya Polisi na Magereza pamoja na TAMISEMI wamekutana na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini DPP akiwa pamoja na wataalamu wake kwa lengo la kuangalia mafanikio na changamoto zilizojitokeza wakati wa kutenganishwa kwa shughuli za uendeshaji wa mashitaka mahakamani na masuala ya Upelelezi.
Wakizungumza katika mkutano huo kwenye Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, Wataalamu hao wamesema kuwa mchakato huo umeleta manufaa makubwa na kwamba kwa kiasi Fulani umepunguza msongamano wa kesi mahakamani na wafungwa na mahabusu magerezani.
Naibu Mkurugenzi wa mashitaka nchini Bi. Winfrida Koroso, akitoa taarifa kwenye mkutano huo amesema kuwa Idara yake imeweza kupanua wigo wa kiutendaji na kwamba katika mikoa minane walioanza kuendesha mashtaka kutoka Jeshi la Polisi wamepata mafanikio makubwa.
Akizungumzia mchakato huo, Bi. Koroso, amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa mpango wa huo, Serikali imeongeza ajira kwa mawakili wa Serikali ambao wamewezesha kupunguza msongamano wa kesi mahakamani na hivyo pia kupunguza mlundikano wa mahabusu katika magereza mbalimbali hapa nchini.
Amesema kuongezwa kwa idadi ya mawakili katika mikoa tisa katika mahakama za wilaya na Mahakama za mahakimu wakazi katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Tabora, Shinga, Mbeya na Dodoma.
Amesema tangu kuanza kwa mchakato huo hadi kufikia mwezi Desemba mwaka jana, zaidi ya kesi 10,500 zimemalizika katika mikoa hiyo minane lakini bado mchakato wa kuzifikia wilaya zote 38.
Amesema kuwa kwa mfano mwaka 2008 Magereza ya Tanzania yalikuwa na idadi ya wafungungwa 38,940 na mwaka 2009 37,439 lakini mwaka huu wapo wafungwa wapo 38,239 na bado kuna nafasi zaidi ya kuendelea kupunguza idadi hiyo ya wafungwa na mahabusu magerezani.
Naye Mkurugenzi wa mashitaka nchini DPP Bw. Eliaza Feleshi, amesema kuwa kukutana kwa vyombo hivyo vya dola kunawawezesha kujua mafanikio na mapungufu yaliyojitokeza tangu kuzinduliwa bwa Jukwaa la haki sheria mwishoni mwa mwaka jana.
Hata hivyo Bw. Feleshi ametaka mikutano kama hiyo ifanyike hadi kufikia ngazi ya wilaya kwa watendaji wa kada hiyo kuendelea kukutana na bubadilishana uzoefu wa kiutendaji.
Amesema kuwa awali mpango huo ulikuwa uanzishwe kwa mikoa sita tu lakini baada ya kuonekana kuwepo na umuhimu Serikali imeona ni vema kupanua wigo na kuanzia katika mikoa minane ya sasa lakini juhudi zinaendelea katika kuhakikisha kuwa mpango huo unapanuka zaidi.
Akichangia hoja katika mkutano huo, Mkuu wa Waendesha Mashitaka kwenye Mahakama ya Kijisutu Jijini Dar es Salaam Bw. Ponsiano Lukosi, amewataka wapelelezi nchini kuendelea kushirikiana na Mawakili wa Serikali ili kuharakisha kupunguza mlundikano wa kesi mahakamani.
Bw. Lukosi amesema kuwa kwa kufanya hivyo kutaiwezesha Idara ya uwendeshaji wa kesi hapa nchini kuongeza tija na kuepuka kuharibika kwa kesi mbalimbali zilizopo katika hatua za mahakama.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, amesema kuwa hakuna mitaji itakayoweza kufanikiwa katika uwekezaji kama nchi haitakuwa na usalama wa kutosha.
Hivyo amesema kuwa ni vema suala la usalama likatiliwa maanani na kuhakikisha kuwa kila eneo kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wanasaidiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha usala wa maeneo mbalimbali yakiwemo yale wanayoishi ama yenye miradi ya uwekezaji.
Akitoa taarifa katika mkutano huo, mwakilishi wa Jeshi la Magereza nchini ambaye pia ni mwanasheria wa Jeshi hilo, SSP Geroge Mwambashi, amesema kuwa msongamano wa mahabusu na wafungwa katika magereza mbalimbali hapa nchini, kunatokana na kukosekana kwa huduma hiyo katika wilaya zilizoanzishwa bila kuzingatia umuhimu wa miundombinu hiyo.
Katika mkutano huo pia umehudhuriwa na Wakili wa serikali Mwandamizi kutoka TAMISEMI Bw. Suleimani Lukanga, Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Upelelezi nchini kamishna Robert Manumba, Mwakilishi wa Mkuu wa magereza nchini Naibu Kamishna kamugisha Muganyizi na Mwanasheria mshauri kamishna Laurian Tibasana toka Ofisi ya Mwendesha Mashitaka eri Mkuu.

0 comments:
Post a Comment