Vogts ataka Fifa imsaidie kuidai Nigeria!!

Kocha wa Zamani wa Nigeria Mjerumani Bert Vorgts.
Kocha mkongwe, Berti Vogts, amerejea Fifa kutaka shirikisho hilo la soka duniani kuchukua hatua dhidi ya chama cha soka cha Nigeria, NFF, kimlipe fedha anazokidai.
Licha ya madai ya kocha huyo aliyewahi kuifundisha Super Eagles, mkuu wa NFF, Sani Lulu amesisitiza kuwa swala hilo lilishapatiwa ufumbuzi siku mbili zilizopita.
Miezi minne iliyopita, Fifa iliagiza NFF kumlipa mjerumani huyo kiasi cha fedha ambacho hakikutajwa kama mshahara wake alipokuwa akiifundisha timu ya taifa ya Nigeria.
Huku muda uliopangwa wa siku 30 ukiwa umemalizika majuma manane yaliyopita, NFF bado haijalipa fedha hizo, Stefan von Moers mwanasheria wa Vogts alidai.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment