LINA MHANDO MGENI RASMI MASHUJAA SUNDAY SOCCER BONANZA!!


Mabingwa wa kwanza katika michuano ya Maveterani MASHUJAA SUNDAY BONANZA, Timu ya Mabibo jumapili hii imepangwa kucheza na timu ya Scud Veterani ya Mtoni katika mchezo wa nne katika Viwanja vya Ukonga Magereza.
Kwa mujibu wa mratibu wa michuano hiyo Spia Mbwembwe, mchezo wa kwanza utazikutanisha timu za New Ukonga itakayocheza na timu ya Kipunguni kutoka kundi A, mchezo utakaoanza majira ya saa tatu kamili asubuhi.
Mchezo wa pili utakuwa kati ya timu ya Segerea Veterani dhidi ya timu ya Scud Veterani Mtoni B, na mchezo wa tatun uitazikutanisha timu za Wizara ya Afya itakayomenyana na timu ya Kipunguni kabla ya timu ya Mabibo Veterani ambao wameendelea kushiriki bonanza hilo baada ya kuwa bingwa wa Mashindano ambayo itacheza na Scud Veterani Mtoni.
Mchezo mwingine utakuwa dhidi yab New Ukonga dhidi ya Wizara ya Afya, Segera dhidi ya Mabibo Veterani.
Akizungumzia utaratibu wa michuano hiyo spia alisema kuwa sheria kumi na saba zitatumika, ambapo timu zote zitapaswa kuwa na nidhamu ikiwa ni pamoja na wachezaji, Viongozi na Mashabiki.
Aidha timu itakayosababisha fujo itaondolewa katika Bonanza, ambapo kila wiki jumla ya timu sita zitashiriki, na timu tatu zitagawiwa kila kundi A na B, na timu mbili kila kundi zitafuzu hatua ya nusu fainal ambazo zitacheza kwa mtoano na kama azikufungana timu hizo zitapigiana penalt tatu tatu na suluhu ya mwisho itakuwa kurusha shilingi endapo zimemaliza zikiwa zimefungana.
Washindi wa kwanza na pili kila wiki watapata fulsa ya kushiriki katika bonanza linalofuatia, na kila mchezo utachezwa dakika 25 kila kipindi na dakika 50 kwa mchezo mzima, na kwamba mchezaji atakayepatiwa kadi nyekundu anaruhusiwa kuendelea na mchezo unaofuata isipokuwa kama amepewa kwa ajili ya ugomvi atafungiwa kushiriki bonanza hilo.
Zawadi za mchezaji bora, Mfungaji Bora , Kipa bora, Mwamuzi bora, Mfungaji wa Goli la kwanza wa kila wiki, wote wameandaliwa zawadi ikiwa ni pamoja na Zawadi ya mshindi wa kwanza ambaye yeye atachukua mbuzi(Mnyama), na zawadi ya mshindi wa Pili Creti moja la bila.
Burudani kabambe itatolewa na kundi la Muziki la Mashujaa Musica Band chini ya kiongozi wao Elyston Angai, ambayo itakuwa katika bwalo la maafisa wa magereza ambapo kila timu itaruhusiwa kuingiza wachezaji 16 na wengine watachangia kiasi cha shilingi 2000 kila mmoja na wanawake wote ni bure.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment