Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi Saidi Magalula, Mkurugenzi wa Mfuko huo Mwamvita Makamba alisema kwamba msaada huo ni mwendelezo wa awamu ya tatu ya Mradi wa Ugawahi kompyuta kwa shule za sekondari za vijijini. Katila awamu ya kwanza na ya pili jumla ya shule 30 kutoka mikoa tofauti 15 zilifaidika katika mradi huu.
Alisema huu ni mwanzo tu kwani Vodacom Foundation itaendelea kutoa misaada ya kompyuta katika shule za mikoa mbalimbali hapa nchini ikiwa unalenga kutoa wimbi la uduni wa kompyuta na kuinua elimu na kuisaidia serikali kama sekta binafsi siyo kuiachia serikali pekee lazima tuwe pamoja kuendeleza misingi iliyobora ya elimu. Naye Mkuu wa Wilaya, akipokea msaada huo aliishukuru kampuni ya Vodacom kupitia mfuko wake huo na kusema sera ya ushirikishwaji wa sekta binafsi katika kutoa misaada mbalimbali ya kuiokoa jamii kama Vodacom ni mfano wa kuigwa na mashirika mbalimbali ili waweze kuisaidia serikali na wananchi wanaopatwa na upungufu wa vitu muhimu katika jamii.
“Serikali imeweka sera nzuri za uwekezaji ili kuhakikisha kwamba uwekezaji una kua na wawekezaji pia wanapata fursa ya kuchangia maendeleo ya sekta ya kijamii nchini’
Alisema hivi sasa bila teknolojia ya kisasa amna maendeleo na alichukua frusa hiyo ya kuwaasa wanafunzi wazitunze kompyuta hizo na kuzitumia vizuri kwani wameunganishwa na ulimwengu wa teknolojia ya kisasa na kuwasihi wasitembelee katika tovuti zenye mambo yasiyofaa na ambayo hayana manufaa kwao.
0 comments:
Post a Comment