NA MAGRETH KINABO- MAELEZO
21/03/2010
WIZARA ya Maji na Umwagiliaji iko katikamchakato wa kutafsri sheria za mjai kwa lugha ya Kiswahili ili wannachi waweze kuzielewa na kuzifuata.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Naomi Lupimo kutoka Idara ya Maji na Umwagiliaji wakati akitoa mada kuhusu athari za uchafuziwa vyanzo vya maji kwa viumbe hai na myzamo wa sheria mpya za maji katika kuzuia uchafuzi kwenye warsha ya siku moja ya wadau wa maji iliyofanyika kwenye Shirika la Elimu Kibaha.
“Tuko katika mchakato wa kuzibadilishwa sheria za maji kwa lugha ya Kiswahili ili tuweze kuzisambaza kabla ya mwaka ujo wa fedha sasa hivi tunaendelea kutunga sheria ndogondogo kwa ajili ya ufafanuzi wa sheria hizo, “ alisema Lupimo.
Akizungumzia kuhusu sheria hizo, Mwanasheria wa Wizara hiyo, Sabina Faya alisema ni Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za vyanzo vya Maj namba 11 ya mwaka 2009 na Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira namba 12 ya mwaka 2009, ambazo tayari zimeshaanza kutekelezwa kuanzia Agosti Mosi mwaka huu.
Naye Mwanasheria mwingine wa wizara hiyo, Gloria Chegeni alisema katika Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za vyanzo vya Maji namba 11 ya mwaka 2009, kifungu cha 39- 42 kinasema adhabu inapatikana kwenye kifungu cha 103 a,mbapo mtu atakayeikiuka faini ni sh milioni moja na isiyozidi milioni 10 au kigungo kisichozidi miezi sita aya mika miwili au vyote yaani faini na vifungo
0 comments:
Post a Comment