Rufaa ya Algeria Kombe la Dunia yatupwa!!


Shirikisho la Soka la Algeria (Faf) limeshindwa rufaa yake ya Kombe la Dunia inayohusiana na kutenguliwa adhabu ya kufungiwa Nadir Belhadj na Faouzi Chaouchi.

Mapema mwezi huu, Shirikisho la Sola la Afrika (Caf) liliwafungia Belhadj kucheza michezo miwili na Chaouchi kucheza mechi tatu.

Lakini Caf imeendelea kushikilia msimamo wake wa adhabu hiyo iliyotoa kutokana na utovu wa nidhamu.

Wachezaji hao wawili waliadhibiwa kwa kuoneshwa kadi nyekundu katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Angola mwezi Januari walipofungwa mabao 4-0 na Misri.

Mlinzi Rafik Halliche pia alitolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo huo na yeye amefungiwa kucheza mchezo mmoja.

Wachezaji hao watatu wamekwishatumikia adhabu ya kutocheza mchezo mmoja, kutafuta nafasi ya tatu Kombe la Mataifa ya Afrika, Halliche anaweza kucheza michezo yote ya kundi C Kombe la Dunia, ila Belhadj anayechezea Portsmouth hatocheza mchezo wa ufunguzi na Slovenia.

Hata hivyo, Algeria italazimika kucheza michezo yake miwili ya awali dhidi ya Slovenia na England bila ya mlinda mlango wao nambari moja Chaouchi.
WWW.BBCSWAHILI.COM

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment