TIMU ZA NETBALL ZATAKIWA KUJITOKEZA MASHUJAA SUNDAY BONANZA (MALASUSA)!


Timu za mpira wa wa pete (Netball) wanawake zimetakiwa kujitokeza kushiriki katika mabonanza kama ilivyo kwa timu za Wanaume (Mpira wa Miguu) kwa lengo la kukuza na kujenga mahusiano ikiwa ni pamoja na kujenga mwili kupitia Mazoezi.
Hayo yamesemwa juzi na Mgeni rasmi katika bonanza la kila wiki kwenye Viwanja vya Magereza Ukonga Bi. Christina Malasusa wakati akifunga bonanza hilo kwenye Bwalo la Maafisa wa Magereza Ukonga ambako timu mbalimbali za Veterani kwa upande wa mpira wa miguu zilishiriki na Mabibo Veterani kuibuka na ushindi na kuibuka mna zawadi ya Mbuzi.
Bi. Christina Malasusa alisema kuwa, anazipongeza timu zote shiriki katika bonanza la (Mashujaa Sunday Bonanza) kwa kuweza kujitokeza kwa wingi kushiriki na kwamba wazidi kufika wakati mwingine kwani Michezo hujenga undugu, ushirikiano na pia huwafanya washiriki kuwa na afya njema.
“Ninawapongeza na kuwashukuru wote mlioweza kujitokeza mahala hapa hii leo, pengine bila nyinyi yawezekana hata shughuli hii isingeweza kufanikiwa, isipokuwa niseme jambo moja kwenu, kwamba nimefuhi kuona Bonanza hili likimalizika bila kuwepo na purukushani za aina yoyote pamoja na kwamba wengi wenu mlikuwa mkiendeleza kinywaji tangu majira ya mchana, ni jambo la kujivunia sana, na pengine niwaombe ndugu zangu kwamba, wakati mwingine nyinyi kina baba, hakikisheni mnabeba wake zenu ili mshiriki pamoja katika bonanza wao wakiwa katika Netball nyinyi mnakuwa katika Football, hii itawawezesha kuzijenga Familia zenu na kuwa za Ukakamavu, zenye kujumuika na wengine, na pia itatusaidia sisi kina mama kuzidi kuendeleza pia Fani yetu ya mchezo huu wa Netball” alisema Christina.
Katika bonanza hilo Bendi mpya ya kisasa katika ulimwengu wa burudani ya Rhumba, Sebene, Shoo, Dansi ya MASHUJAA MUSICA ilikuwa ndiyo gumzo kutokana na vitu ilivyoonyesha ikiwa ni pamoja na kutoa shoo kabambe ambayo ilionekana kuwachengua maelfu ya watazamaji waliokuwa wamejitokeza kushuhudia burudani ya Mpira wa Miguu na Pia kushuhudia Burudani ya Bendi hiyo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment