Klabu yaTottenham inajiandaa kukamilisha mipango ya kumsajili kiungo wa Kimataifa kutoka Brazil aitwaye Sandro.
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo kupitia tovuti yake imesema makubaliano yanakamilika kumsajili Mbrazil huyo kuanzia msimu ujao.
Sandro mwenye umri wa miaka 21 atafanyiwa uchunguzi wa afya wiki hii kabla hajarejea Brazil kumalizia msimu wa ligi ya kwao.
Meneja wa Spurs Harry Redknapp amesema"Tuna matumaini yote yatakamilika sasa na utakuwa usajili mzuri. Ameendelea kumsifu" Ni mchezaji hodari ambaye bado kijana."
Hata hivyo mkataba ili ukamilike kunahitajika kibali cha kufanyia kazi kwa sababu mchezaji huyo hajiimarisha katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil, ingawa aliichezea mara moja tu mwezi wa Septemba mwaka 2009 walipocheza na Chile katika mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia.
0 comments:
Post a Comment