Tiba ya damu kwa bei nafuu yapatikana

Dawa ya ugonjwa wa damu (lukemia) inayotumiwa kwa kumeza iliyotengenezwa huko Hongkong imekuwa ya kwanza kusajiliwa nchini Marekani kutokana na kiwango cha mafanikio yake.
Kundi la madaktari wa chuo kikuu cha Hong Kong walifanikisha dawa hio ya tembe ijulikanayo kama arsenic trioxide. Dawa hio imetumiwa kutibu wagonjwa wa mji huo wenye aina fulani ya lukemia kwa ufanisi mkubwa. Kutokana na ufanisi huo yumkini ni bora kuliko tiba ya saratani ya kubadilisha uboho wa mfupa au tibakemikali.
Huko Marekani dawa ya kutumia mirija inagharimu hadi dola elfu mbili kwa tiba ya kila siku. Hata hivyo wataalamu wa Hongkong wanasema dawa hii mpya haitogharimu kiasi kama hicho na wataituma kwa wagonjwa wa nchi zinazoendelea bila malipo.
Dawa hii imefanyiwa majaribio 100 huko Hong Kong tangu mwaka 2000 na kati ya wagonjwa 56 ambao kabla ya hapo maradhi hayo yaliwasimbua mara kwa mara, 55 hawakusumbuliwa tena.
Uwezekano wao kuweza kupona ulitazamiwa kuwa asili mia 70, kiwango cha juu kuliko wagonjwa waliotibiwa kwa njia za kubadili uboho wa mfupa au tibakemikali.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment