Kutoka kushoto Prof. Hermas Mwansoko,Suleiman M.Hegga mwenyekiti (BAKITA),Mh.George Mkuchika Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Mikutano wa DICC,wa Miwsho ni Dk.Anna Kishe Katibu mtendaji (BAKITA).
Baraza la Kiswahili la Taifa BAKITA,leo limezinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam likiambatanisha na utoaji wa yeti kwa wajumbe wa baraza lililopita.
Akizungumza katika uzinduzi huo mgeni Waziri wa Utamaduni Habari na Michezo Mh.George Mkuchika amesema,anatumia sheria ya Bunge ya mwaka 1967 kifungu namba 7 kuchagua wajumbe watakaolitumikia Baraza kwa muda wa miaka 3 yaani 2010-2013.
Aidha Mh.Mkuchika amesisitiza umuhimu wa kutumia Kiswahili kwa usanifu badala ya kupotosha jamii,kwa kutumia Kiswahili vibaya tofauti na jinsi inavyotakiwa.
Pia Mh.Mkuchika amesema kuna baadhi ya makampuni ambayo yametumia Kiswahili katika wingi hata wakati neno hilo halina wingi wake,Mabango ya barabarani yameandikwa kwa lugha ya Kiingereza kwa asilimia 70 wakati waandikiwa na wasomaji ni waswahili na lugha yao ni ya Kiswahili.
Mh.Mkuchika amewataka pia wakuu wa vyombo mbali mbali vya Habari kutafuta mtu anayefahamu Kiswahili na kukaa kama Marehemu Omar Jongo ili kuweza kuchambua habari zinazoandikwa kwa lugha ya Kiswahili fasaha ili zisipotoshe jamii,mfano matumizi ya neno “FISADI” lenye maana ya mtu anayechukua wake za watu wengine lakini vyombo vya habari vimelitumia vibaya na kupotosha jamii.
Akihitimisha katika uzinduzi wa Baraza hilo la Kiswahili Waziri Mkuchika amesema,leo Watanzania wako katika mfumo wa Ukoloni Mamboleo Mning’inio kwani asilimia 70 ya matangazo ni ya Kiingereza wakati wasomaji karibu Milioni 40 ni Watanzania na wanatumia Lugha ya Kiswahili Je wataelewa?

0 comments:
Post a Comment