Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Serengeti Breweriers Ltd Imani Lwinga kushoto akikabidhi Mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 12 kwa mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communication Co. Ltd Maria Sarungi ambao ni wandaaji wa Miss Universe Tanzania kulia na katikati ni Miss Universe Tanzania 2009 Illuminata Jemsi, ikiwa ni udhamini wa shindano la Miss Universe 2010.
Shindano hilo mwaka huu linatarajiwa kuanza kuanzia katika mikoa ya Morogoro tarehe 27 mwezi machi 2010 , 28 Mjini Dodoma, 31 mjini Mwanza, tarehe 6 aprili Arusha na shindano hilo litahitimishwa kwa kufanya mashindano ya mkoa wa Dar es salaam tarehe 9-10 aprili kabla ya fainali zinazotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi wa Nne zikishirikisha warembo 20 watakaopatikana katika mashindano hayo ya mikoa.
Katika kuboresha mashindano hayo tayari Mshindi wa mwaka jana Illuminata Jemsi ameshapata udhamini kutoka chuo cha New York Film Academy cha Marekani ambako atasomea masuala ya uigizaji wa filamu au utangazaji na mshindi atakayepatikana tena mwaka huu atapata nafasi ya kusoma katika chuo hicho.
Wadhamini wa Miss Universe Tanzania 2010 ni PSI, Precision Air, Choice Fm, Movenpick, New York Film Academy, Prime Time Promotion na Hugo Domingo.
0 comments:
Post a Comment