Waziri a Habari ,Utamaduni na Michezo George Mkuchika akiongozana na Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali TSN Wilson Mukama (kulia) leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Bodi ya TSN . Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.
Benjamin SaweMaelezoDar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Mheshimiwa George Mkuchika amewataka wanahabari kuwa mstari wa mbele katika kuelimisha Watanzania juu ya sheria mpya ya matumizi ya fedha katika kipindi cha uchaguzi. Aliyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Bodi mpya ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania (TSN) jana ambapo aliwataka wanahabari kuelimisha wananchi juu ya haki yao ya kuchagua kiongozi bora. Aidha Mheshimiwa Mkuchika aliishauri Bodi mpya ya Kampuni la TSN isione uvivu kuwapeleka watumishi wake masomoni ili kuongeza ujuzi wa kazi ili waweze kutumika kikamilifu baada ya kumaliza masomo yao. Mheshimiwa Mkuchika alisema Bodi hiyo inachangamoto kubwa ya kuhakikisha utawala wa TSN unazingatia sheria,kanuni na maagizo ya Serikali ili kuepusha migogoro mahali pa kazi. Waziri Mkuchika alisema Wizara imeikabidhi Kampuni ya magazeti ya TSN kwa bodi hiyo mpya ili ikabiliane na changamoto mbalimbali hususani katika jukumu kubwa la kuhabarisha na kutoa elimu kwa ummaPia aliitaka Bodi hiyo kusimamia utendaji wa TSN na kubuni mbinu nzuri zaidi za utendaji ikiwa na kubuni vyanzo vingine vya mapato ili kuongeza mapato ya shirika na kuepuka utegemezi wa Serikali.Mheshimiwa Mkuchika aliiomba Bodi mpya ya Shirika la TSN kufuatilia kwa karibu mapato na matumizi ya Kampuni hiyo ili kukwepa hati chafu ya ukaguzi wa mahesabu na kuwataka kuwa safi katika mahesabu yao kila mwaka.Nae Mwenyekiti wa Bodi mpya ya TSN Bwana Wilson Mukama alisema watashirikiana na Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo ili kuhakikisha Shirika la magazeti la TSN linasonga mbele na kuongeza mapato kwa kuanzisha vyanzo vingine vya mapato.Mheshimiwa Mkuchika ameteua Bodi mpya ya TSN ambayo inaongozwa na Mwenyekiti Wilson Mukama, wajumbe ni Clement Mshana ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari,Bwana Charles Rajabu,Hajat Mmanga na Bi Kalua Simba ambapo bodi hiyo itadumu kwa miaka mitatu.
Waziri wa Habari ,Utamaduni na Michezo George Mkuchika (kulia) akiongea na Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya TSN leo jijini wakati wa uzinduzi. Mwengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya TSN Wilson Mukama.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya magazeti ya Serikali TSN Wilson Mukama (miwani) akibadilishana mawazo jijini leo Dar es salaam na Mjumbe wa Bodi ambae pia ni Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO) Clement Mshana (katikati) akifuatiwa na Kaimu Mhariri Mtendaji waTSN Mkubwa Ally.(kulia) kabla ya uzinduzi wa Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali.
0 comments:
Post a Comment