Na Mohammed mhina, wa Jeshi la Polisi
Watu kumi wakiwemo Askari Polisi wanane na watoto wawili ambao ni familia za askari mkoani Tabora wamejeruhiwa na wengine kulazwa katika hospitali ya Mkoa Tabora na Nzega kwa matibabu baada ya Gari la Polisi walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka.
Kaim Kamanda wa Polisi mkoani Tabora SSP Anthony Rutta, amesema kuwa ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 9.30 arasili huko kwenye kijiji cha Kilino kilichopo katika kata ya Insanzu wilayani Nzega baada ya Gari la Polisi lenye namba PT 1512 aina ya Land Rover Pick Up ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia FFU mkoani Tabora ikiendeshwa na Konsetbo Godfrey wa Kikosi hicho kuacha njia na kuanguka.
Kamanda Rutha amewataja askari waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Inspeta Lusatila, F. 6495 PC Geofrey ambaye alikuwa dereva wa gari hilo, E.1043 CPL Nkwabi, F.3632 PC Kaitira, F.9832 PC Alex, G.3448 PC Omari, G.2403 PC Richard, na G.4246 PC Abuu.
Amewatara Raia waliojeruwa katika ajali hiyo kuwa ni Idrisa Musa Mguha ambaye ni mtoto wa Mkuu wa Polisi wilaya ya Nzega SSP Mussa Mguha na Enock Kaitira ambaye ni motto wa asari aliekuwa akirejea nyumba na baba yake akitokea shuleni Nzega.
Hata hivyo amesema kuwa hali za askari na watoto hao zinaendelea vizuri na wengine walitibiwa na kuruhusiwa kurejea kambini.
Amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa mpira wa tairi la gurudumu la nyuma upande wa kushoto kusababisha gari hilo kuyumba na kuanguka pembeni mwa barabara.
Kamanda Rutha amesema Gari hilo lilipinduka wakati likiwarejesha askari mjini Tabora baada ya kumaliza zam yao ya ulinzi katika Mgodi wa Dhahabu wa Rusu uliopo wilayani Nzega, Mgodi ambao unaomilikiwa na Makaburu.

0 comments:
Post a Comment