Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais wa Namibia Hifikepunye Pohamba katika hafla maalumu kuadhimisha miaka 20 ya Uhuru wa Namibia na pia kushinda uchaguzi mkuu ambapo ataendelea kuiongoza Namibia kwa muhula wa pili.Sherehe hizo zilifanyika katika mji mkuu wa Namibia Windhoek.
Rais Wa Namibia Hifikepunye Pohamba akimkabidhi Nishani ya Juu ya Ushujaa ya Taifa la Namibia, Mama Maria Nyerere kwa niaba ya Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa kutambua juhudi za Mwalimu katika ukombozi wa bara la Afrika ikiwemo Namibia katika hafla maalumu iliyofayika katika mji mkuu wa nchi hiyo Windhoek.

Katika hafla hiyo viongozi Mbalimbali wa Afrika waliokuwa mstari wa mbele katika harakati za ukombozi kusini mwa Afrika nao walitunukiwa nishani hiyo akiwemo Rais wa Zamani wa Zambia Keneth Kaunda ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, Marehemu Agostino Neto wa Angola, Marehemu Oliver Tambo wa Afrika ya Kusini, Rais Denis Sassou Nguesso wa Kongo Brazaville, pamoja na watu wengine mashuhuri waliokuwa msari mbele katika ukombozi wa bara la Afrika.Pembeni ya Mama Maria kushoto ni Mtoto wa Mwalimu,Bwana Makongoro Nyerere ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mara.
0 comments:
Post a Comment