Uuzaji wa pembe za ndovu kuamuliwa!!

Nchi wanachama wa shirika la Umoja wa mataifa la hifadhi ya mimea na wanyama walio katika hatari ya kutoweka duniani watapiga kura kuamua iwapo nchi za Afrika zitauza shehena ya pembe za ndovu.
Mkutano huo unaoendelea katika mji wa Doha, nchini Qatar, unatokana na vuta nikuvute kati ya nchi zenye ndovu wengi barani Afrika.
Tanzania ina pembe za ndovu zenye thamani ya dola milioni 20 za kimarekani ambazo ingependa kuuza. Afrika Kjsini na Zambia zimeunga mkono Tanzania.
Kenya inapinga biashara ya pembe za ndovu ikidai hatua hiyo itawavutia majangili kuingia mbuga za wanyama wa pori na kuua ndovu na wanyama wengine.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment