Mahakama yathibitisha ushindi wa Rais Gnassingbe!!

Rais Faure Gnassingbe wa Togo.

Mahakama ya katiba nchini Togo imethibitisha ushindi wa rais Faure Gnassingbe, kufuatia uchaguzi uliotawaliwa na mizozo mapema mwezi huu.
Upinzani ulipinga matokeo ya uchaguzi huo ukidai kura ziliibiwa. Kumekuwa na maandamano katika maeneo kadhaa katika mji mkuu wa Togo Lome, tangu matokeo ya awali ya uchaguzi huo yalipotangazwa yapata siku 10 zilizopita.
Rais Gnassingbe alimrithi bababe marehemu Eyadema Gnassingbe, kama rais wa nchi hiyo mwaka wa 2005, lakini ushindi wake wa kwanza uligubikwa na ghasia, ambazo zilisababisha vifo vya mamia ya watu nchini humo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment