Balozi wa India Nchini Tanzania K.V Bagirath wa pili kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Samsung Miss Tanzania India Richa Adhia wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika leo jioni nyumbani kwa balozi Oysterbay jijini Dar es salaam, Richa Adhia anaondoka jumapili kwenda nchini Afrika Kusini ambako anatarajiwa kushiriki kwenye shindano la Miss India Worldwide litakalifanyika katika jiji la Durban machi 27/ 2010, hii ni mara ya kwanza kwa Mtanzania mwenye asili ya india kushiriki katika shindano hilo lililoanzanishwa mwaka 1990,wengine ni mbunifu wa mavazi Mustafa Hassanali na Kiltda Patel mfanyabiashara mashuhuri nchini FULLSHANGWE inamtakia kila mafanikio mshiriki huyo kutoka Tanzania ili aweza kufanya vyema na kuipeperusha bendera ya Tanzania.
Mbunifu wa mavazi nchini Mustafa Hassanali na baadhi ya wageni waalikwa wakipozi kwa picha mbele ya Camera ya FULLSHANGWE katika hafla ya kumuaga Samsung Miss Tanzania India Richa Adhia nyumbani kwa balozi wa India.
Mshauri wa balozi masuala ya habari na Utamaduni Sanjeev Manchanda akibadilishana mawazo na Samsung Miss Tanzania India Richa Adhia wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika nyumbani kwa balozi Oysterbay jijini Dar es salaam leo jioni.
Balozi wa India Nchini Mh. K.V Bhagirath wa pili kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Samsung Miss Tanzanian India wa tatu kushoto pamoja na maafisa wengine wa ubalozi wa india na waratibu wa Samsung Miss Tanzania India pamoja na wageni waalikwa wenginea katika hafla ya kumuaga mrembo huyo iliyofanyika nyumbani kwa balozi. Oysterbay jijini Dar es salaam leo jioni.
0 comments:
Post a Comment