KILO 3.5 ZA DAWA ZA KULEVYA AINA YA HEROINE ZAKAMATWA!!



Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi


Jeshi la Polisi Kitengo cha Kuzia Dawa za Kulevya nchini, kimefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja aitwaye Abdallah Dhoul-Kelly Awadhi(29), akiwa na kiasi kikubwa cha dawa za kulevya aina ya Heroine yenye uzito wa kilo 3,5 zenye thamani ya karibu shilingi milioni 100.

Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya nchini ACP Godfrey Nzowa, amesema kuwa mtuhumiwa huyo amekamatiwa huko Tabata kwenye Bonde la Msimbazi baada ya Makachero wa Polisi kuivamia nyumba yake na kuendesha upekuzi wa ghafla baada ya kupata taarifa toka kwa Raia wema juu ya kuwepo kwa dawa hizo.


Amesema Polisi walikuwa wakiifanyia kazi taarifa hizo na kwamba leo Machi 20, 2010 walipata uhakika wa kuwepo kwa dawa hizo pamoja na mtuhumiwa ambaye bado anahojiwa na makachero wa kitengo hicho.

Amesema dawa hizo zimekamatwa zikiwa tayari zimeshafungwa kwa kusafirishwa ama kuingizwa katika soko la jumla kabla ya kusambazwa kwa watumiaji.

Kamanda Nzowa amesema kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa akiwa na Hati ya kusafiria ambapo inaonyesha kuwa tangu alipoipata mwaka 2008 mtuhumiwa huyo amekuwa na safari za mara kwa mara za kati ya Tanzania na China.

Amesema bado Makachero wake wanaendelea na mahopjiano ili kubaini Genge la mtuhumiwa huyo pamoja na mtandao wake unaojihusisha na madawa hayo.


Amesema Dawa hizo Kamanda Nzowa amesema Hiyo ni mara ya pili kwa Jeshi la Polisi kukamata kiasi kikubwa cha Dawa za kulevta. Ambapo Machi 8, mwaka huu huko Kabuku wilaya Handeni katika mkoa wa Tanga Polisi waliwakamata watu sita wakiwa na kilo 95 za Dawa za kulevya aina ya Heroine.

Kamanda Nzowa ameendelea kutoa wito kwa Watanzania kuendelea kulisaidia Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa zenye uhakika ili wahalifu wa makosa mbalimbali wakiwemo wale wa dawa za kulevya watiwe mbaroni na kushitakiwa.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Raia tuacheni roho mbaya ,hayo madawa yote yataishia Mitaani,Mnawapa Polisi ulaji wa bure, ROHO MBAYA TU.

Post a Comment