Akizungumza na kamanda wa FULLSHANGWE katika uwanja wa ndege wa Malimu K.K.Nyerere kabla ya kupanda ndege mwanamuziki mkongwe wa bendi hiyo Bob Ludala amesema maonyesho hayo yanashirikisha wanamuziki 40 kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Amezitaja nchi hizo kuwa ni Afrika Kusini, Zimbabwe, Ethiopia, Bokinafaso, Kenya Tanzania na Ivory Coast ambao wanakutana pamoja na kufanya maonyesho hayo katika mataifa mbalimbali ya bara la Ulaya.
Amewataja wanamuziki ambao wanaondoka katika kundi hilo kuwa ni mpiga Saxphone Khamis Mulenge, Solo Gitaa Nurdin Makimu, Bass gitaa Roy Fiquiredo, Conga Ras Pompydue, Drums Richard Mwanisawa, Keyboard Bisman na Muimbaji ambaye ni Bob Ludala mwenyewe. katika picha ni baadhi ya wanamuziki Bob Ludala mwenye kofia kushoto na Bisman wa pili kutoka kulia wakiwa na wenzao.
0 comments:
Post a Comment