FULLSHANGWE NA MATUKIO YA SIMBA KUTOKA ZIMBABWE MPAKA J.K.NYERERE ASUBUHI HII!!

Juma K. Juma Golikipa wa Simba akihojiwa na Mtangazaji wa TBC1 Malyo Ndejengwa mara baada ya timu ya Simba kuwasili asubuhi hii ikitokea Zimbabwe ambako ilicheza jana jioni na timu ya Leigthens kwenye uwanja wa Rufaro jijini Harare na kushinda magoli 3-0 katika michuano ya kombe la shirikisho la CAF timu hizo zitarejeana tena baada ya wiki mbili jijini Dar es salaam. FULLSHANGWE ilikuwepo eneo la tukio na inakuletea matukio yote kuanzia kwenye mchezo wa jana jioni mpaka kuwasili kwa timu hiyo kwenye uwanja wa Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dar es salaam pata mambo katika picha mdau
Juma Kaseja golikipa wa Simba akisalimiana na mashabiki mara baada ya wachezaji hao kuwasili asubuhi hii kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere wakitokea nchini Zimbabwe.
Mfungaji wa goli la pili Mohamed Banka mbele na Juma Jabu JJ wakitoka nje huku mashabiki wakiwashangilia nmara baada ya kuwasili leo asubuhi.
Mustafa Barthez wa simba akitoka nje mara baada ya kuwasili na timu yao asubuhi hii.
Marafiki wa Timu ya Simba kutoka kulia ni Majaliwa Mbasa, Kassim Dewaji, Salim Try Again na Nick Magarinza.
Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia wakati wa mapokezi ya timu ya Simba iliyowasili asubuhi hii ikitokea nchini Zimbabwe.

Kocha mkuu wa Timu ya Simba Mzambia Patrick Phiri akihojiwa na mtangazaji wa BBC mara baada ya mchezo huo kumalizika na Simba kushinda kwa magoli matatu dhidi ya wazimbabwe wa Leigthens jijini Harare jana jioni.
Kapten wa timu ya Simba Nico Nyagawa akitolewa nje na wafanyakazi wa msalaba mwekundu baada ya kuumia kwenye mchezo huo.
Muss Hassan Mgosi kulia akimtungua goli la kwanza golikipa wa Leigthens aliyelala golini.

Kikosi cha Simba vijana wa Patrick Phiri.

Kikosi cha timu ya Leigthens ya Zimbabwe ambayo jana ilibugizwa magoli 3-0 na Simba.

Timu Zikiingia uwanjani tayari kwa kuanza mpambano huo katika uwanja wa Rufaro jijini Harare jana jioni.

Kaburu Nyange kulia na Nick Magarinza wakipeperusha bendera kama ishara ya ushindi kabla ya mchezo huo kuanza.
Mwanafullshangwe Nick Magarinza aka (Nick But) akishangilia goli huku wanahabari kutoka vyombo mbalimbali na mashabiki wakiangalia.

Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe Adadi Rajabu wa pili kulia mtari wa nyuma akiwa pamoja na mwenyekiti wa Simba Hassan Dalali mwenye kofia pamoja na viongozi wengine wa Simba na Shirikisho la soka nchini TFF wakiangalia mchezo kati ya Simba na Leigthens ya Zimbabwe jana jioni.
Mwenyekiti wa kamati ya Usajiri ya Simba Kassim Dewaji mwenye suti ya bluu akiwa na marafiki wengine wa Simba wakifuatilia kwa karibu mchezo huo jana.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment