Capello amwalika Beckham Afrika Kusini!!

David Bekham.

Kocha wa England Fabio Capello amemualika David Beckham kujiunga na kikosi cha England cha Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini licha ya kiungo huyo kuwa ameumia.
Capello ameiambia televisheni ya Gol "Tumemwambia Beckham aambatane nasi kuelekea Afrika Kusini."
Ameendelea kufahamisha"Inategemea na yeye mwenyewe na namna jeraha lake lilivyo. "Ni wazi hatoweza kucheza kwa sababu itambidi asubiri kwa miezi sita."
Beckham alifanyiwa upasuaji siku ya Jumatatu nchini Finland, lakini nahodha huyo wa zamani wa England mwenye umri wa miaka 34, hatokuwa katika nafasi ya kucheza Afrika Kusini.
Capello pia amesema bado mlizi wa kushoto wa Mnchester City Wayne Bridge anayo nafasi kufikiria upya uamuzi wake wa kuichezea England.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment