Timu ya Simba leo imedhihirisha ubora wake ndani ya jiji la Harare nchini Zimbabwe baada ya kuikung'uta timu ya Leighthens magoli 3-0 katika mchezo ambao Simba ilicheza kiwango cha hali ya juu wakati timu hizo zilipokutana katika mashindano ya Kombe la washindi barani Afrika.
Akizungumza kwa njia ya simu MWANAFULLSHANGWE aliyeko Zimbawe kwa ahili ya kushuhudia mchezo huo amesema timu ya Simba imecheza kwa kujiamini katika kipindi chote cha mchezo huku wenyeji wakiomba mpira uishe kutokana na mashambulizi yaliyokuwa yakielekzwa langoni mwao.
Magoli mawili ya Simba yamefungwa katika kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi na lile la pili limefungwa na kiungo mshambuliaji Mohamed Banka huku Simba ikicheza kwa kujiamini na kasi kwa muda wote wa mchezo mpaka kipindi cha kwanza kilipomalizika.
Katika kipindi cha pili Leigthens wamejaribu kutaka kuzuia mashambulizi bila mafanikio kwa katika dakika za lala salama mchezaji wa simba Mohamed Kijusu mtambo wa kubadili mchezo ameifungia timu ya Simba goli la Tatu katika dakika ya 89 ya mchezo goli ambalo liliwamalizia kabisa wazimbabwe hao hivyo matumaini yao ya kusonga mbele katika michuano hiyo kuwa finyu zaidi mara timu hizo zinatakaporejeana jijini Dar es salaam wiki mbili zijazo. mpaka mwisho wa mcjhezo Simba3 Leigthens 0
0 comments:
Post a Comment