FULLSHANGWE IKIWA JIJINI HARARE INAKULETEA MOJA KWA MOJA MATUKIO YA MPAMBANO KATI YA SIMBA NA LEIGTHENS RUFARO STADIUM!!

Kikosi cha Simba kikipasha misuli kabla ya mpambano wake kati yake na timu ya Legthens ya Zimbabwe jijini Harare katika michuano ya kombe la shirikisho yanayoandaliwa na shirikisho la soka barani Africa CAF mchezo huo unachezwa jioni hii na Blogu yako ya FULLSHANGWE ambayo iko katika uwanja wa Rufaro jijini Harare kuripoti matukio ya mchezo wa Simba na Leigthens na itakuwa ikikuletea moja kwa moja matukio ya mchezo huo kadiri myetishaji wake Nick Magarinza aka (Nick Butt) atakavyokuwa akishusha taarifa kutoka huko mdau kaa mkao wa kula Fullshangwe iko kwa ajili yako.

Mzambi Patrick Phiri Kocha wa Simba ambaye pia anachukuliwa kama kocha bora afrika mashariki kwa mwaka huu akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mazoezi kabla ya kuikabili timu ya Legthens ya Zimbabwe katika kombe la Shirikisho mjini Harare.

Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya usajiri ya Simba Kasim Dewaji na kulia ni Nick Magarinza pamoja na viongozi na wadau wengine wa Friends of Simba wakiangalia mazoezi ya timu hiyo kabla ya mchezo wake leo jijini Harare Zimbabwe.

Wacezaji wa Timu ya Simba wakijifua kwenye uwanja wa Rufaro Stadium ambako pambano hilo litachezwa kati ya simba na Leigthens ya Zimbabwe leo.

Kasim Dewji mwenye kanzu akiwa pamoja na Mulamu Ng'ambi kushoto na Salimu Try Again pamoja na wanasimba wengine kabla ya timu kwenda mazoezini jana jioni.


Wadau wa SSC wakiwa kwenye ofisi za Ubalozi wa Tanzania jjijini Harare. Mwenye suti nyeusi na Tai kulia ni kaimu Balozi Ndg. Isaack Mwakiluma akiongea na wadau wa Simba pamoja na viongozi mbalimbali walioongozana na timu

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. tunasubiri kwa hamu kubwa kama vile mwenye njaa ya kufunga anaponusa harufu ya pilau.

Post a Comment