(EWURA CCC) YATOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma zanishati na maji EWURA CCC Mhandisi Prof. Jamidu Katima akizungumza nawaandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kwenye maonyesho ya wikiya maji yanayofanyika kwenye kijiji cha Mwendapole Kibaha Mkoani Pwaniwakati alipozungumzania changamoto mbalimbali zinazolikabili barazahilo katika juhudi zake za kuhakikisha watumiaji wa huduma hizowanapata huduma bora, maadhimisho hayo mwaka huu yanafanyika kitaifamkoani Pwani huku kauli mbiu ikiwa ni "Maji safi na salama kwa afya bora".

BARAZA LA USHAURI LA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA NISAHTI NA MAJI (EWURA CCC)
USHIRIKI WA BARAZA KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI 2010
UTANGULIZI
Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji limeungana na Wizara ya Maji na Umwagiliaji na wadau wengine wote wa maji kuadhimisha Wiki ya Maji Duniani, maadhimisho yaliyoanza tarehe 16/03/2010 na yanatarajiwa kufikia kilele mnamo tarehe 22/03/2010. Kaulimbiu ya Wiki ya Maji kitaifa mwaka huu ni Maji Safi na Salama kwa Afya Bora.
MALENGO YA BARAZA KUSHIRIKI
Moja ya malengo ya Baraza ni kutoa taarifa sahihi kwa watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA kuhusu masuala mbalimbali yanayowahusu watumiaji wa huduma hizo kwa lengo la kukuza ufahamu wao na kuwajengea uwezo wa kujenga hoja zenye mantiki pindi inapowalazimu kufanya hivyo. Hivyo basi, ushiriki wa Baraza katika tukio la kitaifa kama hili ni fursa nzuri ya kukutana na wadau ili kutoa mwamko, kupokea changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa ajili ya kuzifanyia kazi, kupokea maoni, kujibu dukuduku kwa kukutana nao uso kwa uso. Pia ni wakati mwafaka kutambua uelewa wa watumiaji wa Nishati na Maji.
Pia ushiriki wa Baraza katika jukwaa kama hili kunatoa fursa nzuri kwa Baraza kutoa elimu kwa umma kuhusu uwepo wa Baraza hili, kazi zake na kutoa maelezo ya kina kuhusu dhana nzima ya udhibiti kwani dhana hii bado ni ngeni masikioni pa watumiaji wengi, na hivyo juhudi za makusudi kuuelimisha umma wa watanzania zinahitajika.
Baraza kwa upande mwingine linatumia nafasi hii kuwaelimisha watumiaji na wadau wengine wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA kuhusu haki na wajibu wao katika mchakato mzima wa kupata huduma husika, na hasa tukizingatia kuwa asilimia kubwa ya watanzania wana ufahamu mdogo kuhusu haki na wajibu wao hata inapotokea wao kugandamizwa na watoa huduma aidha kwa kutokupewa huduma stahili au kwa kunyimwa haki ya kupewa taarifa kuhusu masuala yanayowahusu n.k.
UHUSIANO ULIOPO BAINA YA WIKI YA MAJI NA MAJUKUMU YA BARAZA
Mataifa mbalimbali duniani kila mwaka hujumika kutafakari njisi ya kukabili changamoto za sekta ya maji kila tarehe 22 Machi. Wanafanya hivyo lengo kuu likiwa ni kuwasikiliza walaji na wadau wa sekta ya maji. Watetezi wa walaji hawa ni mabaraza yanayoundwa kwa minajili ya kufatilia hoja zinazomlinda mlaji na kumweleze wajibu wake. Haya huwezekana kwa njia ya tafiti mbalimbali na ufahamu wa kimtaifa. Kwa mfano, suala la viwango ni mlinzi sahihi wa mtumiaji.
EWURA CCC ni mdau mkubwa wa malaji, yaani mtumiaji wa maji, na mtumiaji wa maji ni watu wote, wakiwemo waandishi wa habari, wajumbe wa Baraza, wanafunzi, wasomi, watoto, watu wazima, lakini pia viumbe hai kama mimea, wanyama na wadudu wote uhai wao hutegemea maji. Pasipo maji hakuna uhai.
Kaulimbiu ya Wiki ya Maji mwaka huu 2010 ni “Maji Safi na Salama kwa Afya Yako”. Kaulimbiu hii ina uhusiano wa moja kwa moja na shughuli ama majukumu ya Baraza kwa kuwa tunapozungumzia Maji, moja kwa moja Baraza linahusika na masuala ya maji kwani pia ni sekta inayodhibitiwa na EWURA.
Pili, Moja ya haki ya msingi ni kupata huduma za msingi ambazo zinajumuisha maji ambayo sharti yawe safi na salama kwa matumizi ya binadamu na viumbe hai vinavyomilikiwa na wanadamu, kwamba haki hiyo ikitokea ikakosekana sharti watumiaji waidai.
Tatu, haki nyingine tunayowaelimisha watumiaji ni ile ya kupata huduma ya maji salama kwakuwa, maji yasiyokuwa salama yanasababisha matatizo kwa mtumiaji kama vile kuhara n.k. Kwahiyo basi, unaweza kuona wazi shughuli tunazozifanya kama Baraza zina uhusiano wa moja kwa moja na kaulimbiu ya wiki ya maji mwaka huu 2010.
CHANGAMOTO ZILIZOBAINIKA KWA BARAZA TOKA KUANZA KWA MAADHIMISHO HAYA YA 22
Kama ilivyo kawaida kwa matukio ya kitaifa na hata yale yasiyo ya kimataifa, changamoto huwa hazikosekani. Toka tulivyoanza kushiriki katika maadhimisho haya Jumatatu tarehe 16/03/2010, na mpaka sasa tukiwa na siku tatu mbele yetu tumebaini kuwa mambo mengi yanajirudia kila siku ya maadhimisho, kadhalika yapo mambo mbalimbali kimsingi yanaonekana ya manufaa kwa Baraza, yaani badala ya kuwa changamoto yanaonekana kama fundisho katika kutekeleza dira na malengo ya Baraza. Hata hivyo kila kukicha tunapata sura mpya za watu wa rika na tabaka mbalimbali. Zipo changamoto kadhaa lakini kiujumla ni kama ifuatavyo:-
i) Upo mwamko mdogo wa wananchi kushiriki maadhimisho kwa dhamira ya kujifunza.
Kimsingi upo umati wa makundi mbalimbali ya watu uliojitokeza kufika katika maonesho tuliyonayo. Lakini ushiriki hadi leo hii tunapotoa taarifa hii si wa kuridhisha.
Washiriki kwa idadi yao kundi kubwa lililojitokeza ni rika la umri mdogo ambao wengi wao maisha yao bado tegemezi. Kundi hili japo ni jepesi kujifunza kwa mbinu za kudadisi lakini hupenda kujifunza vitu tofauti na huduma bora na haki ya mlaji katika sekta hii muhimu ya maji, na kwa sababu si jambo linalogusa sana shughuli za maisha yao ya kila siku. Hata pale waliposhiriki watu wazima imeonekana baadhi yao, japo kwa uchache hudiriki kuhitaji mavazi ya fulana (T- Shirt) kuliko kuhoji elimu kuhusu haki zao na wajibu wao kuhusu sekta ya maji. Ni watu wachache sana wanaokuwa na hamasa ya kuelimishwa kwani wengine hupita mabandani kwa kuangalia tu picha na kusikiliza muziki na shamrashamra za vikundi vya utamaduni. Pengine hii ni changamoto kubwa siyo kwa Baraza tu bali pia kwa sisi Baraza, wizara na wadau ambao ndiyo waandaaji wa maadhimisho haya.
Hoja ya msingi hapa ni kubuni mbinu za ziada za makusudi kuuelimisha umma wa watanzania kwa kupitia njia mbalimbali za mawasiliano. Hoja ya ushiriki hafifu basi inatokana na Uelewa mdogo miongoni mwa watumiaji wa huduma ya maji kuhusu dhana nzima ya udhibiti, wajibu na haki ikiwa ni pamoja na kuyajua majukumu ya Baraza.
ii) Malalamiko kuhusu huduma duni ya maji kwa wakazi wa maeneo ya Kibaha.
Kibaha ndipo yanapofanyikia maadhimisho haya ya Wiki ya Maji. Mathalani malalamiko na vilio vingi tulivyokumbana navyo hapa ni wateja kwa kilipia huduma wasiyoipata kila mwezi na wengine kupata maji yasiyo na kiwango (maji meusi) bila kujua cha kufanya. Tatizo hili lilikuwa kubwa siku za nyuma, lakini mamlaka zinazohusika zinaendelea kutatua tatizo hilo, hasa maeneo ya miradi mipya halipo tena.
MIKAKATI ILIYOPO KUKABILIANA NA CHANGAMOTO HIZI
Baraza limejipanga kuimarisha kampeni zake za kujitangaza na kuzifanya endelevu kwa lengo la kujitangaza na kuendelea kutoa elimu kuhusu masuala yanayomhusu mtumiaji kupitia njia mbalimbali za mawasiliano kama vile vyombo vya habari; kwa mantiki hii ninyi ni wadau wakubwa wa jamii tuliyonayao. Hakuna njia ya mkato ya kuleta mwamko wa kutosha kwa watumiaji wao wenyewe, hivyo kuwa kichocheo chanya cha kuleta mabadiliko ya haraka katika sekta ya maji kwa kujua wajibu wao na kutetea haki zao; hilo ndilo jukumu letu EWURA CCC , kuwa watumiaji wawe na mwamko wa kutosha na kuzijua njia sahihi ya kudai haki zao.
Majukwaa (forum) na matukio mengine ya kitaifa na kimataifa – kama tulivyo leo – ni fursa mahsusi ya kutoa elimu kwa umma na hivyo kukaribisha mabadiliko ya kweli na haraka.Mbinu nyingine ni kuendelea kutumia majukwaa mengine kama sanaa mbalimbali, viongozi wa mikoa na taifa ili kuwaelimisha watumiaji wa huduma hizi juu ya wajibu na haki zao.
Mbele yetu sisi kama Baraza tumeona mara moja umuhimu wa kutoa Ushauri kwa Wizara na Kamati ya maandalizi ya maadhimisho haya juu ya kubuni mbinu mpya ya kuwahamasisha wananchi ili kuitika kwa wingi zaidi kushiriki Wiki ya Maji Duniani ili walaji, wadau na serikali kwa ujumla kutumia fursa hiyo kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya maji.
Imetolewa na
MHANDISI PROF. JAMIDU KATIMA
MWENYEKITI, BARAZA LA USHAURI LA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA NISHATI NA MAJI (EWURA CCC) TAREHE 19/03/2010.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment