Rais Jakaya Kikwete
Na Veronica Kazimoto – MAELEZO.
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Meja jenerali mstaafu Ligathe Sande kuwa mwenyekiti wa Bodi ya chuo cha Bahari (DMI) kwa kipindi kingine cha miaka mitatu. Taarifa iliyotolewa na Katibu mkuu wa Wizara ya Miundombinu Mhandisi Omar Chambo imesema kuwa, Ligathe Sande ameteuliwa kwa mara ya tatu baada ya kushika wadhifa huo kwa kipindi cha miaka sita iliyopita na kuongeza kuwa uteuzi huo ulianza tangu tarehe 10 februari, mwaka huu. Wakati huo huo Waziri wa Miundombinu Dkt Shukuru Kawambwa ameteua jumla ya wajumbe sita ambao ni wawakilishi kutoka Serikalini na Asasi mbalimbali kuunda bodi hiyo ya chuo cha Bahari. Wajumbe hao ni Bi Tumpe Mwaijande mwakilishi kutoka Wizara ya Miundombinu, Bwana David Lwimbo kutoka Ikulu na Meja generali Said Omar kutoka Jeshi la wananchi kikosi cha Wanamaji. Wengine ni Bi Tumaini Silaa kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), Bwana Primus Nkwera kutoka Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE – National Council for Techinical Education) pamoja na Bi Rukia Shamte kutoka Chama cha Wakala wa Forodha (TFFA – Tanzania Freight Forwaders Association).
0 comments:
Post a Comment