Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amewasili Mashariki ya Kati kwa lengo la kujaribu kufufua mazungumzo ya amani kati ya Israel na Wapalestina.
Ziara yake inatokea wakati matumaini ya kufanyika kwa mazungumzo ya pande hizo mbili yakionekana kufifia.
Kwanza atazuru mjini Ramallah katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel, na baadaye atakutana na viongozi wa Israel.
Bw Ban huenda akatumia matamshi makali kuhusu suala kubwa linaloleta mgawanyiko, ambalo ni hatua ya Israel ya kukataa kusitisha ujenzi wa makaazi mapya ya walowezi wa Kiyahudi Mashariki mwa Jerusalem na katika maeneo mengine ambayo yanakaliwa kimabavu na Israel.
Hatua hiyo imewakasirisha Wapalestina, ambao wamesema hawatokuwa tayari kushiriki mazungumzo ya amani, hadi hapo uamuzi huo ubatilishwe.

0 comments:
Post a Comment